Makonda aingilia kati kivuko Kujengwa MURIET

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda leo Aprili 15,2025 ametembelea Mtaa wa Muriet uliopo katika Kata ya Sokoni 1 kufuatia malalamiko ya Wananchi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa ahadi ya kujengwa kwa kivuko kinachounganisha Kata za Muriet, Sinoni na Lemara nakuagiza kivuko cha muda kianze kwa haraka kuanzia kesho Aprili 16,2025

April 14,2025 AyoTV iliripoti habari ya malalamiko ya Wananchi wa eneo hilo wakilalamika kuwa kivuko hicho chenye urefu wa mita 15 kutoka darajani hadi mtoni kinachotumiwa na zaidi ya watu 2,000 kwa siku wakiwemo Wanafunzi zaidi ya 300 wanaokwenda Shule kila siku kuharibika na kuoza baada ya kujengwa na nguvu za Wananchi wenyewe.

“Pasaka watu wanaweza wakala wakiwa wanapita bila kuwa na shida,hiyo ni zawadi ya paska kutoka kwa Rais Dkt Samia suluhu Hassan,”-Makonda

Makala Nyingine:

INEC ifute tamko kuwa CHADEMA Haishiriki Uchaguzi