INEC ifute tamko kuwa CHADEMA Haishiriki Uchaguzi

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala ameitaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kufuta tamko lake linalosema kuwa CHADEMA haitoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 na chaguzi ndogo zijazo ndani ya miaka mitano kwasababu ya kutosaini kanuni za maadili.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo April 15,2025, Nshala amesema “Haki ya kuchaguliwa kuwa Mgombea inatolewa na Katiba, alichokisema Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ni makosa makubwa yamekiuka sheria ya nchi, yamekiuka katiba na yamekiuka hata kanuni ambazo hazijaanza kufanya kazi, Mtu anabanwaje na kanuni ambazo hazijaanza kufanya kazi?”

“Ndugu Kailima tafadhali naomba ujitazame mara mbili kasome kanuni vizuri uone usahihi wa maneno yako”

“CHADEMA haijabadilisha msimamo inadai reforms, kilichofanywa na Kailima ni propaganda chafu, tunataka kama dhamira zao ni safi na akili zao zinafanya kazi wafute hilo tamko , Kailima amekosea na atoke hadharani aseme kama alivyonukuliwa akisema CHADEMA haitoshiriki uchaguzi kwasababu haijasaini kanuni za maadili, kwakuwa kauli hii inapingana na Katiba, aondoe na afute kauli hiyo, sisi CHADEMA msimamo wetu uko palepale no reforms no election”

“Huu uchaguzi ulivyo bila reforms tukiingia tumepigwa, CCM ni kama wamechukua madume, na majike yote kwahiyo wewe ukienda umepigwa, ni set up game, hatuwezi kuwa na Viongozi wanaotokana na uhuni na wizi wa kula, hatuwezi kuwa na uchaguzi wa ujanja ujanja, haikubaliki”

Makala Nyingine: