Sifa za kujiunga na JWTZ (Jeshi La Wananchi Wa Tanzania)

Sifa za kujiunga na JWTZ (Jeshi La Wananchi Wa Tanzania) Vigezo vya Kujiunga na Jeshi La Wananchi, Utaratibu wa kujiunga na JWTZ, Leo Tutazichambua kwa kina hizi sifa na Vigezo unavyopaswa kuwa navyo ili uweze kuwa moja ya wanaojiunga na Jeshi.

Historia ya kazi na shughuli za ulinzi na usalama hapa Tanzania zilianza tangu zama za mababu zetu. Jamii nyingi zilizoishi katika maeneo mbalimbali hapa nchini zilikuwa na ulinzi wa jadi uliohusisha kila mwanajamii. Ulinzi wa jadi ulikuwa ndiyo msingi wa usalama wa jamii zote kwa wakati ule. Silaha zilizotumika na mababu zetu zilikuwa duni kama vile upinde, mikuki, mundu,mapanga na sime kama silaha za msingi kulinda jamii zao. Kila kabila lilikuwa na namna ya kuwaandaa vijana wao kujifunza matumizi ya silaha na baadaye vijana walipewa jukumu la kulinda jamii zao.

Bara la Afrika lilipata mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii baada ya Mapinduzi ya viwanda yaliyotokea huko Ulaya katika karne ya 19. Mkutano mkuu wa Berlin uliofanyika kuanzia mwaka 1884 hadi 1885 ulifuatiwa na mabadiliko makubwa ya nchi za kiafrika kutawaliwa kisiasa, kiuchumi na kijeshi. Huu ndiyo mwanzo wa nchi nyingi barani Afrika kuanza kuwa chini ya majeshi ya kigeni.

Ujerumani ilijipatia uhalali wa kuitawala Tanganyika baada ya mkutano wa Berlin ulioligawa bara la Afrika katika vipande vya nchi bila ridhaa ya waafrika wenyewe. Jeshi la Kijerumani lilianzisha harakati za kufuta tawala za makabila mbalimbali hapa nchini ili kuwa na utawala mmoja na jeshi moja la kikoloni. Harakati hizo za Wajerumani zilipelekea baadhi ya makabila kupambana na Jeshi la Kijerumani, kwa vile utawala wa kijerumani ulilenga kuharibu mfumo mzima wa ulinzi wa jadi, siasa na uchumi wa wenyeji.

Sifa Za kujiunga na JWTZ

  1. Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: –
  2. Awe raia wa Tanzania
  3. Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
  4. Awe hajaoa/hajaolewa
  5. Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
  6. Awe na tabia na mwenendo mzuri
  7. Awe na akili timamu na afya nzuri

Masharti ya Utumishi

Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.

Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

Maafisa

Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).

Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.

Majukumu ya Msingi ya JWTZ

  1. Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  3. Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.
  4. Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
  5. Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoajiwakati wa maafa.
  6. Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  7. Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.

JWTZ lilianzishwa tarehe 01 Septemba 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru wa nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dira ya JWTZ

Kuwa na Jeshi dogo, shupavu la Viongozi na Wataalamu wenye zana na silaha za kisasa, utayari wa hali ya juu katika ulinzi wa nchi ya Tanzania.

Dhima ya JWTZ

Kulinda nchi na kutetea maslahi ya Taifa la Tanzania, kutoa msaada kwa Mamlaka za kiraia na kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya Kitaifa na Kimataifa.

Makala Nyingine:

  1. JWTZ Vyeo na Mishahara
  2. Jinsi ya Kujiunga na JKT (Mwongozo kamili)
  3. Nafasi za kujiunga na JKT 2025/2026
  4. Sifa za Kujiunga na JKT 2025 Vigezo vya Mafunzo ya Kujitolea
  5. Nafasi za kujitolea JKT Septemba 2024