Nafasi za kujiunga na JKT 2025/2026

Nafasi za kujiunga na JKT 2025/2026  Jinsi YA kujiunga na jkt, Kujitolea www.jkt.go.tz news Nafasi za JKT. Kujiunga kwa mujibu wa Sheria (www.jkt.go.tz 2025/2026 Kujitolea na Kujiunga). Historia ya kuanzishwa JKT inaanzia mwaka 1958 wakati wa ziara ya viongozi wa wa Taifa nchini Ghana, ambapo Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na Mhe. Rashid Kawawa (Simba wa Vita) walikwenda kuhudhuria sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa uhuru wa nchi hiyo.

Wakiwa nchini humo, Mhe. Kawawa alialikwa chakula cha jioni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel, Bi. Golda Meir.

Mhe. Kawawa alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi huyo, ambaye alitanabaisha namna Taifa la Israel linavyowaandaa vijana wake kutumikia Taifa lao kwa moyo wa uzalendo.

Sheria ya Kuanzishwa kwa JKT

JKT ilianzishwa kwa Sheria Namba 16 (National Service Act, 1964) iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 kifungu 3(1). Sheria hii ilipitishwa kuwataka vijana kujitolea kwa hiari kujiunga na JKT ili kulitumikia Taifa. Vijana hao walitakiwa kuwa angalau wawe wamehitimu elimu ya msingi, wanachama wa TYL, wasiwe wameoa au kuolewa na wawe tayari kujitolea kutumikia Taifa kwa muda wa miaka miwili. Baada ya kupitishwa sheria hiyo, Novemba 1964 kundi la kwanza liliripoti Mgulani JKT na kuitwa Operesheni Maendeleo, likiwa na vijana 486.

Kurejeshwa kwa Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria

Kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ilikuwa ni moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele cha juu katika awamu ya nne ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Serikali ya awamu ya nne imerudisha mafunzo ya JKT kwa sababu ya nia njema ya kuendelea kujenga uzalendo kwa vijana wa Tanzania. Itakumbukwa kwamba kutokana na hali ngumu ya kiuchumi Serikali ilishindwa kumudu kuendesha mafunzo ya JKT kwa mujibu. Mnamo Juni 15, 1994 mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria yalisitishwa kwa muda.

Jeshi la Kujenga Taifa limefanya kazi kubwa na nzuri ya kujenga moyo wa utaifa na uzalendo miongoni mwa vijana waliopitia katika Jeshi hilo. Hapa ni mahali ambapo vijana wa itikadi zote, rangi zote, makabila yote, dini zote hukutana, kuishi pamoja na kufanya mafunzo na kazi kama ndugu wa familia moja.

Hakuna chombo chochote cha malezi ya vijana kilichoizidi JKT katika kazi hiyo, pengine hata ile tabia ya Watanzania wengi kutoulizana makabila yao inatokana na uwepo wa JKT. Vijana wazalendo wa Tanzania wanaopitia JKT huwa wanakutana na vijana mbalimbali kutoka kila kona ya nchi yetu, ndiyo maana hawana muda hata wa kuulizana makabila kwa vile wote hujiona ni wamoja.

Jinsi Ya Kujiunga na JKT

Tembelea Page ya http://jkt.go.tz/

Aidha, athari za kusimamishwa kwa mafunzo ya JKT kuliwagusa wengi na ndiyo maana Serikali ya awamu ya nne imerejesha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria. Hatimaye tarehe 26 Machi 2013 mafunzo ya JKT yalianza ikiwa ni pamoja na kutimiza ahadi ya serikali ya kufufua upya mafunzo hayo katika kambi ya Ruvu.

Kama ilivyokuwa mwaka 1964 JKT ilipoanza na mwaka 1968 baada ya mafunzo ya mujibu wa Sheria kuanzishwa viongozi wa kitaifa waliongoza katika kushiriki mafunzo hayo.

Mafunzo hayo ya JKT yalianza na kulikuwa na idadi ya wabunge 22 ambao walishiriki na kumaliza mafunzo ya uongozi. Wabunge hao walitawanywa katika kambi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ya muda wa miezi miwili waliyoomba wenyewe kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo wanaamini yatawajengea uzalendo zaidi kwa taifa lao.

Makao makuu ya Jeshi la kujenga Taifa

S.L.P 2963 DODOMA Tanzania

info@jkt.go.tz

+255 26 2962078

Makala Nyingine:

  1. Sifa za Kujiunga na JKT 2025 Vigezo vya Mafunzo ya Kujitolea
  2. Sifa za Kujiunga na JKT 2025/2026
  3. Nafasi za kujitolea JKT Septemba 2024
  4. Nafasi za Kazi Uhamiaji 2024 Ajira Mpya