Nafasi za Kazi Zimamoto 2025 ajira Jinsi Ya Kutuma Maombi

Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto 2025 ajira zimamoto 2025 Jinsi Ya Kutuma Maombi ajira.zimamoto.go.tz Ajira za,Tangazo la ajira zimamoto 2025/2026 pdf Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania waliohitimu kidato cha nne na ngazi ya shahada. Nafasi hizo zitatolewa kwa ngazi ya Konstebo kwa wale wanaokidhi vigezo vilivyoainishwa.

Taarifa hii imetolewa rasmi leo, Alhamisi, Februari 13, 2025, na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga. Ingawa idadi ya nafasi za kazi haijawekwa wazi, waombaji wanahimizwa kutuma maombi kabla ya tarehe ya mwisho, Februari 28, Mwaka 2025.

Vigezo vya Kustahiki Ajira

Waombaji wanapaswa kukidhi masharti yafuatayo:

Sifa Maelezo
Uraia Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
Umri Miaka 18 – 25 kwa waombaji wa kawaida, 18 – 35 kwa marubani wa helikopta
Urefu Wanaume: Futi 5.7+, Wanawake: Futi 5.4+
Afya Awe na afya njema kimwili na kiakili
Tabia Asiwe na rekodi ya uhalifu, asiwe na tattoo mwilini
Ndoa Asiwe ameoa au kuolewa
Ajira ya awali Asiwe ameajiriwa serikalini hapo awali

Sifa za Ziada kwa Wenye Ujuzi Maalum

Jeshi limeeleza kuwa waombaji wenye taaluma au ujuzi ufuatao wanapewa kipaumbele:

  1. Udereva wa magari makubwa (leseni daraja E, umri miaka 18-28)
  2. Ufundi bomba
  3. Uuguzi
  4. Taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
  5. Utabibu
  6. Urubani wa helikopta

Kwa waombaji wenye shahada, fani zinazopendelewa ni:

  • Uhandisi wa bahari na ndege
  • Lugha (Kiingereza)
  • Ukadiriaji majenzi
  • Teknolojia ya habari
  • Uchumi
  • Sheria (waliomaliza shule ya sheria kwa vitendo)
  • Ualimu
  • Usafirishaji barabara na reli
  • Uhandisi wa kemikali

Jinsi ya Kuomba

Waombaji wanapaswa kutuma maombi kupitia mfumo rasmi wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kiunganishi:

👉 ajira.zimamoto.go.tz

Nyaraka Muhimu za Kuambatisha

  1. Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
  2. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
  3. Fomu ya uthibitisho wa afya kutoka kwa mganga wa serikali
  4. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA
  5. Picha ya pasipoti ya hivi karibuni
  6. Namba ya mtihani wa kidato cha nne

Waombaji wote wanahimizwa kuzingatia vigezo vyote na kutuma maombi kabla ya tarehe 28 Februari 2025.

🔴 Tangazo hili halihusishi malipo yoyote katika mchakato wa kuomba ajira.

Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji au ofisi zao zilizo karibu nawe.

Soma Makala Nyingine:

Fomu ya Uchunguzi wa Afya (PDF)

Nafasi Za Kazi TRA 2025 Ajira Mpya 1592 Zilizotangazwa

Nafasi za Kazi Kutoka MDAs NA LGAs February 2025