Usajili Kwa Watahiniwa Wa Kujitegemea Wa Kidato Cha Pili Na Nne 2025, Tangazo la usajili kwa watahiniwa wa kujitegemea wa kidato cha pili (FTNA) na nne (CSEE) 2025.
USAJILI FTNA CSEE 2025
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watu wote wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA), mwaka 2025 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba;
Kipindi cha usajili kwa Watahiniwa wa Kujitegemea kimeanza tarehe 01/01/2025 hadi 28/02/2025. Ada ya usajili ni Shilingi 50,000/= kwa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 10,000/= kwa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA).
Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01/03/2025 hadi 31/03/2025 watalipa Shilingi 65,000/= kwa ajili ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 15,000/= kwa ajili ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.
Kabla ya kusajiliwa na Mkuu wa Kituo kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye Vituo vya Mitihani kuchukua namba rejea (reference numbers) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada kupitia Benki kwa kutumia ‘Control Number’.
Ufafanuzi kuhusu utaratibu wa hatua za kufuata katika kutengeneza ‘Control Number’ na kujisajili, umetolewa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania: necta.go.tz. Aidha, kwa watahiniwa ambao hawataweza kutumia mfumo huo wapige simu 0738785945 kwa msaada zaidi.
Waombaji wote wasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwani mfumo wa usajili utafungwa mara baada ya kipindi cha usajili kukamilika.
Imetolewa na:
KATIBU MTENDAJI
Makala Nyingine:
- Matokeo ya Kidato Cha Nne 2024/2025 Form Four Results NECTA
- Matokeo Kidato Cha Nne 2024/2025 CSEE Results
- Ratiba ya mtihani form four 2024 Kidato cha nne
- NECTA Yatangaza Matokeo ya kidato cha Pili 2024-2025 (FTNA)
Leave a Reply